MAYANJA ASEMA, YANGA WANA BAHATI SANA
Na Alex Jonas
Kocha wa Simba Sc Jackson Mayanja raia wa Uganda amefunguka na kusema Yanga wana bahati sana hasa baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa ligi kuu bara.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja amesema Yanga ilipata ushindi huo baada ya mchezaji wake Abdi Banda kuonyeshwa kadi nyekundu mwanzoni mwa mchezo.
"Yanga wana bahati sana kwani mwamuzi (Jonnesia Rukyaa) alitutoa mchezoni kwa kitendo chake cha kumpa kadi nyekundu Banda bila makosa yoyote", alisema na kuongeza.
"Mwamuzi aliganya vile ili kututoa mchezoni mapema na kweli tumefungwa, vijana wangu niliwaandaa vizuri nikiamini tutaibuka na ushindi", alisema kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar na Coastal Union.
Simba jana ilichezewa sharubu na vijana wa Jangwani baada ya kuchapwa mabao 2-0 yaliyowekwa kimiani na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe raia wa Burundi