GIANNY INFONTINO RAIS MPYA FIFA
Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la kandanda duniani FIFA leo limempata rais wake mpya atakayerithi nafasi ya Seppt Blatter ambaye ameenguliwa baada ya kuhusishwa na ufisadi mkubwa uliozingira taasisi hiyo kubwa ya soka duniani.
Gianny Infontino ndiye aliyetawazwa kuwa bosi mpya wa shirikisho hilo baada ya kumshinda Al Salman, Infontino alipata kura 115 akimzidi kura 27 mpinzani wake huyo aliyekuwa akiungwa mkono na bara la Afrika.
Infontino alikuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka barani ulaya (UEFA) na anakuwa rais wa tisa wa FIFA baada ya Blatter aliyedumu kwa miaka 18