KWA YANGA HII TAIFA! SIMBA WAKAROGE
Na Alex Jonas
Yanga ililazimishwa sare na Mwadui Fc mjini Shinyanga ya kufungana mabao 2-2 tena ikinusurika kipigo, lakini pia ilipata ushindi kiduchu dhidi ya African Sports ya Tanga uwanja Mkwakwani.
Yanga ikipata bao lake dakika za lala salama, inaonekana Yanga ikicheza nje ya uwanja wa Taifa inakuwa kwenye wakati mgumu msimu huu.
Raundi hii ya pili Yanga ilicheza mechi mbili mfululizo zote ugenini, ilianza kucheza na Caostal Union uwanja Mkwakwani na Yanga ikapokea kipigo chake cha kwanza cha mabao 2-0, pia ikaenda sare na Prosons ya mabao 2-2 uwanja wa Sokoine Mbeya.
Bado imebakiwa na mechi tano za ugenini bila shaka ina kazi ngumu kutetea mwali wake msimu huu, lakini jeshi hilo la Wanajangwani noma sana wakicheza uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Baada ya Yanga kupoteza mechi yake jijini Tanga na kulazimishwa sare jijini Mbeya watu wengi wakahusisha na mgogoro wa chini kwa chini ndani ya kikosi hicho na kupelekea katibu wake mkuu Dk Jonas Tiboroha kujiuzuru.
Lakini iliporejea uwanja wa Taifa ikaishushia kipigo cha mbwa mwizi JKT Ruvu cha mabao 3-0, Simba itakutana na Yanga katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam siku ya jumamosi ijayo.
Simba wanakibarua kigumu kwani jamaa hao wa Jangwani wanajua kuutumia uwanja huo, wana nyota wao kama Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzimxa, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Malimi Busungu na wemginro.
Si kwamba Simba hawawezi kuutumia uwanja huo ila wana kazi ngumu kuwadhibiti Yanga kwani hawajawahi kupoteza mchezo katika dimba hilo na wamekuwa wakitakata muda wote wanapocheza hapo