JOHN WOKA AFARIKI DUNIA
Na Saida Salum
Msanii wa zamani wa kundi la Wagosi wa Kaya John Woka aliyekuwa akiimba muziki wa kizazi kipya amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Muhimbili.
Akizungumza na mwandishi wa blogu hii, kaka wa marehemu Omari Milley amesema mdogo wake amefariki dunia leo alfajili baada ya kupata ajali jana.
John Woka aliyetamba kwa staili yake ya kilevi alipatwa na umauti baada ya jana kuangukiwa na kitu kizito wakati alipokuwa geteji Sinza akitengeneza gari lake.
Marehemu wakati akitengeneza gari lake aliangukiwa na kitu hicho kilichopelekea kulipuka kwa gesi ambayo ilimuathili kichwani kwake baada ya kitu hicho chenye ncha kali kuingia ndani ya ubongo wake na kuchanganyika na damu.
Milley amesema taratibu za mazishi zinapangwa na Mambo Uwanjani itakuwa ikiwajulisha kile kinachotolewa na wafiwa, R.I.P John Woka