STAA WETU: ELIA DANIEL, MSANII WA FILAMU MWENYE NDOTO ZA KUMFIKIA KANUMBA
Na Prince Hoza
KABLA hajaingia rasmi kwenye tasnia ya filamu alikuwa akimuhusudu sana Steven Kanumba (sasa marehemu), Elia aliamini Kanumba ndio msanii bora kwake.
Lakini hilo halizuiliki kwani majuzi tu mwenyekiti wa chama cha wasanii wa filamu Simon Mwakifamba naye alisema hakuna msanii yoyote wa filamu hapa Tanzania aliyemfikia Kanumba hadi sasa.
Elia Daniel naye anatamani japo siku moja anamfikia Kanumba, hilo kwake linahitaji juhudi na maarifa kwani hakuna libaloshindikana chinj ya jua, Elia Daniel ni muigizaji wa filamu za kibongo ama Bongo Movie, ni mzaliwa wa mkoani Mbeya miaka 28 iliyopita mwezi Agosti, tarehe 27.
Katika mazungumzo yake na blogu hii, Elia (pichani, kulia akiwa na Masinde) alianza rasmi kujikita kwenye filamu mwaka 2002 mkoani Mbeya na anasema amekutana na changamoto nyingi mpaka kufikia hapo halipo sasa.
Ameshashiriki filamu nyingi za wasanii wenzake kipindi hicho akiwa bado hajaweza kumudu vema sanaa hiyo, 'Nilikuwa bado sina uwezo wa kutengeneza filamu zangu ila namshukuru mungu kwa yote' alisema Elia baba wa mtoto mmoja.
Elia anasema soko la filamu Tanzania limekuwa gumu japo amefanikiwa kutoa filamu zilizoingia sokoni, ' Nimetengeneza filamu zangu mwenyewe ambazo ni Secret Life, Segere Mtaa na Sadaka na zote hizo zipo madukani' anasema.
Elia ni muigizaji na pia ni muongozaji na mtayarishaji filamu ambaye anaamini ipo siku atafungua kampuni yake mwenyewe ya kutengeneza filamu.
Kuhusu bifu, Elia anasema yeye hana bifu na msanii yeyote licha ya kuenezwa taarifa kuwa aligombana na rafiki yake Kimlola Kimlola jambo ambalo si kweli.
'Watu walitaka kunigombanisha na Kimlola, yule ni rafiki yangu kikazi siwezi kugombana naye, lakini zinavumishwa habari kuwa sina maelewano naye jambo ambalo si kweli' analalamika Elia Daniel ambaye anadai zamani alijulikana kwa jina la Elly G