KASSIM MAPILI KUZIKWA IJUMAA, KUMBE ALIKUFA KWA PRESHA, BARCELONA YAHUSISHWA

Na Mwandishi Wetu

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kassim Mapili amwfariki dunia jumanne iliyopita kwa maradhi ya shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa mkwe wa marehemu, Wema Mustafa Mgombelwa 'Baba wawili' amesema shughuri za mazishi ya marehemu mzee Kassim Mapili zinafanyika Magomeni Mapipa mtaa wa Magomeni namba 21.

Wema alisema wanaweza kumzika katika makaburi ya Mwinyimkuu au Kisutu jijini Dar es Salaam (leo Ijumaa).

Mkwe huyi ambaye ni seneta wa bendi ya Msondo Ngoma alisema mkwe wake alifariki jumanne usiku baada ya kutoka kuangalia mchezo wa mpira wa miguu kati ya Arsenal na Barcelona.

"Kikubwa alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu, alifariki usiku na maiti tuliipeleka Muhimbili baada ya kupata taarifa za msiba huo, tunawaomba ndugu jamaa na marafiki kujumuika pamoja katika mazishi ya mzee wetu", alisema Wema.

Marehemu Kassim Mapili alijipatia umaarufu mkubwa enzi zake akikung' uta gitaa la solo, pia alikuwa mwimbaji mahiri, Mungu ailaze roho yake mahara pema peponi, Amina


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA