MAONI: NITASHANGAA SANA KAMA TFF ITAZIACHIA GEITA GOLD NA POLISI TABORA BILA KUZIFUNGIA
Na Prince Hoza
NI dhahili kabisa matokeo yamepangwa, hakuna ligi yenye ushindani mkubwa kama ligi Daraja la kwanza Tanzania bara (FDL).
Lakini cha kushangaza timu zinapigwa 8-0 na nyingine 7-0 halafu mechi za mwisho ambazo zinaamua nani apande ligi kuu bara, Geita Gold Mine inayonolewa na nchezaji wa zamani na kocha msaidizi wa Simba Sc Seleman Matola iliitungua JKT Kanembwa ya Kigoma mabao 8-0.
Huo ulikuwa mchezo wa mwisho ambao umeiwezesha Geita Gold kupanda ligi kuu bara, wakati Geita ikiichapa Kanembwa, Polisi Tabora nayo ikaichapa JKT Orjolo mabao 7-0.
Polisi nayo ilihitaji ushindi mkubwa kama huo ili iweze kuungana na Ruvu Shooting na Aftican Lyon ambazo tayari zimeshapanda ligi kuu bara.
Ushindi mkubwa wa Geita Gold na ule wa Polisi Tabora si kwamba naupinga kwa chuki binafsi, hapana, Geita Gold naifahamu sana ni timu yenye uwezo mkubwa wa kusakata kandanda na inao uwezo wa kushinda mabao mengi kama hayo.
Si mara ya kwanza klabu za ligi kuu kukubali vipigo kama hivyo, tulishuhudia Coastal Union ikifungwa mabao 8-0 na Yanga msimu uliopita, lakini sote tuliridhika na kipigo hicho.
Hakuna shaka ypoyote kwenye ushindi huo wa Yanga, tuliamini kiwango chao kilistahili kupata matokeo hayo, Geita Gold nayo naiheshimu sana.
Inacheza vizuri na iliwahi kuifunga Simba mabao 3-1 mchezo wa kirafiki, lakini kinachonisikitisha ni kupata ushindi mkubwa kwenye mchezo wa mwisho ambao walihitaji mabao kama hayo ili wapande ligi kuu.
Kwa vyovyote TFF itapinga kwa nguvu zote matokeo hayo na njia nzuri ya kufanya ili kuondoa mizozo mechi hizo mbili zote zirudiwe katika viwanja vingine.
Ama ikibainika kweli wamepanga matokeo basi hakuna shaka timu hizo zote nne zilizopanga matokeo zishushwe daraja, nitashangaa sana kama TFF itaziachia Geita na Polisi na kubariki matokeo yao kwani naamini kabisa ligi Daraja la kwanza ina ushindani mkubwa kuliko hata wa ligi kuu bara.
TUONANE WIKI IJAYO