Kesho ni "Derby" ya Tabora, Milambo na Msange JKT
Na Emil Kasapa. Tabora
Timu ya soka ya Milambo FC maarufu kama wanazuke mselebende wanatarajia kushuka dimbani kesho katika uwanja wa Mwinyi mkoani hapa kucheza mchezo wao wa watano wa ligi daraja la pili dhidi ya Msange JKT zote kutoka mkoani Tabora.
Timu hizo zinakutana huku Milambo ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 9 wakati Msange Jkt (mabingwa wa mkoa huu msimu uliopita) wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 5.
Kuelekea mchezo huo mwenyekiti wa Msange JKT Pascal Francis amesem wamejipanga kuhakikisha wanapunga gape pa pointi kati yao na ndugu zao Milambo.
Kwa upande wake msemaji wa kikosi cha wanazuke mselebende-Milambo Fc ,Ramadhan Faraji amesema makosa waliyoyafanya katika mchezo dhidi ya mashujaa na kuppteza hayatajirudia tena kesho.