Bila Aishi Manula, Mnyama alikuwa anachinjwa kirahisi jana
Na Saida Salum. Dar es Salaam
#Michezo: BILA AISHI MANULA MNYAMA JANA ALIKUWA ANACHINJWA KIRAHISI.
Mlinda mlango namba moja kwa sasa hapa nchini, Aishi Salum Manula jana amefanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya wachezaji wa Yanga iliyokuwa inaelekea moja kwa moja wavuni.
Yanga jana ilikutana na hasimu wake Simba katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1, Simba walitangulia kupata bao likifungwa na Shiza Kichuya lakini dakika mbili baadaye Yanga wakakomboa kupitia kwa Obrey Chirwa.
Lakini kama si juhudi za Aishi Manula ambaye alikuwa golikipa wa Simba basi huenda mnyama angelala mapema tena si chini ya bao nne, kwani wachezaji wa Yanga walikuwa wanalenga langoni kwa kupiga mashuti makali.
Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DRC jana alikuwa hatari kwa Simba baada ya kufanikiwa kupiga mashuti mawili makali ambayo yaliokolewa na Manula, Manula anatajwa kama mchezaji bora wa mechi hiyo kwa upande wa Simba, wachezaji wengine waliomjaribu ni Geofrey Mwashiuya, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na wengineo