MKALI FIZO AACHANA NA UKAPERA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyetamba na wimbo wake "Mapenzi ujinga", Fadhili Kimbendela "Mkali Fizo", Jumamosi iliyopita aliuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mchumba wake, Bi Mariam Khalifa iliyofanyika nyumbani kwake Tabata Dar es salaam.
MKALI FIZO (KULIA) NA MKEWE BI MARIAMU KHALIFA (KUSHOTO) WAKIWA KATIKA FURAHA ILIYOJE BAADA YA KUFUNGA NDOA
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mkali Fizo amefurahia harusi yake hiyo na kudai mwenyezi Mungu amemjaalia mpaka kuitimiza ndoto yake ya muda mrefu.
Fizo ambaye ni msanii wa bongofleva akiwa tayari ameshaachia nyimbo nne hewani, amedai kikubwa kwake anachokisubiria katika ndoa yake ni kuishi kwa amani na upendo na kupata familia bora, naye mke wa msanij huyo Bi Mariamu Khalifa amemsifu mumewe kuwa ni mume bora kwake kwani anampenda na ndio maana amekubali kuolewa naye