YANGA YAIENDEA SIMBA, MORO
Na Ikram Khamees. Morogoro
Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga SC imeingia kambini rasmi jana mjini Morogoro ikiwa tayari kabisa kuchuana na mahasimu wao Simba SC, Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga, Dissmas Ten amethibitisha kikosi hicho kuwasili jana Morogoro kikitokea Shinyanga na basi lake, hata hivyo Ten amedai wavhezaji wake watatu ambao iliwaacha Dar es Salaam kwa maana Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko nao wameungana na wenzao kambini hapo.
Yanga yenye pointi 15 na mechi saba sawa na mahasimu wake Simba SC ambao wako kileleni kwa tofauti ya magoli ya kufunga, itangia uwanjani ikitaka kulipiza kisasi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wa Ngao ya Jamii uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Agosti 23 mwaka huu