WACHEZAJI MBEYA CITY WAAPA KUFA NA SIMBA JUMAPILI
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Wachezaji wa kikosi cha Mbeya City wamesema watakula sahani moja na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC watakapokutana Jumapili ijayo mchezo wa ligi raundi ya tisa.
Mbeya City ambayo ilifingwa bao 1-0 na Azam FC katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam wameapa kufia uwanjani ili wasifungwe na Simba na kugeuzwa ngazi ya ubingwa.
Simba ambayo Jumamosi iliyopita ililazimishwa sare ya 1-1 na watani wao wa jadi, Yanga SC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, nao hawatakubali kupoteza mchezo huo hivyo itazifanya nyasi za uwanja wa Sokoine kuwaka moto.
Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa ameiambia Mambo Uwanjani kuwa wanaisubiri kwa hamu kubwa mechi hiyo ili wathibitishe kile wanachokisema