KUELEKEA MPAMBANO WA WATANI, SIMBA WAMUHOFIA AJIBU
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kuelekea mpambano wa watani wa jadi Jumamosi ya keshokutwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, baadhi ya viongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wameanza kumuhofia mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe alisikika akisifu uwezo wa Ajibu na akawahi kusema katika kikosi cha Yanga anayemnyima usingizi ni Ajibu peke yake, wakati Hanspoppe akimlilia Ajibu, mwanachama na shabiki lialia wa Simba, Said Muchacho naye amesema Ajibu ndio anamyima raha.
Na leo hii aliyekuwa mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage naye ameonyesha hisia zake kwa Ajibu akisema anaweza kuwalaza mapema ingawa Rage ameenda mbali kwa kusema Yanga si lolote kwao na watawafunga na Ajibu wao.
Ajibu alikuwa mchezaji wa Simba na tangu ajiunge na Yanga amekuwa na mwanzo mzuri ambapo mpaka sasa amekuwa akiifungia timu yake hiyo mabao muhimu, mpaka sasa Ajibu amefunga magoli matano akiwa nyuma ya kinara wa mabao Emmanuel Okwi