Simba yatangulia Zenji kuifanyia ukatiri Yanga
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC leo asubuhi wameelekea visiwani Unguja kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na pambano la mahasimu litakalofanyika Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara amesema, Simba imewasili Zanzibar mapema na itakaa huko kwa juma moja kabla ya kucheza na mtani wake Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara, vinara hao waliishinda Njombe Mji mabao 4-0 Junamosi iliyopita.
Huo utakuwa mchezo wao wa tatu mwaka huu kukutana mahasimu hao na mara mbili Simba imeibuka mbabe, mara moja ikishinda 2-1 uwanja wa Taifa mchezo wa marudio wa Ligi Kuu bara na maya ya pili mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba pia ikishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare tasa 0-0 dakika tisini za mchezo