HUYU TSHISHIMBI ALIWAVURUGAVURUGA SIMBA JANA

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Inaaminika kwamba Papy Kabamba Tshishimbi ndio mchezaji bora wa mechi ya jana ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na timu hizo kufungana bao 1-1.

Tshishimbi jana alikuwa akionekana kila ulipo mpira kwa maana alizunguka uwanja mzima, na pia yeye alifanya kazi ya ziada kukata umeme na kuwapoteza viungo wote wa Simba.

Kama si uhodari wa kipa wa Simba Aishi Manula, basi jana Tshishimbi alikuwa anafunga mabao yake mawili saafi, Tshishimbi aliwavurugavuruga Mzamiru Yassin, James Kotei na kufanya wasionekane kabisa uwanjani mpaka kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Omog akaamua kuwatoa

Papy Kabamba Tshishimbi aliwavurugavuruga viungo wa Simba jana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA