Prisons yazidi kuikandamiza Ruvu Shooting ya Masau Bwire
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya
Timu ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Bao pekee lililoizamisha Ruvu Shooting ya Masau Bwire lilifungwa na straika Mohamed Rashid mapema kabisa dakika ya 19 kipindi cha kwanza, na kwa ushindi huo Prisons imefikisha pointi 13 sawa na Singida United na ikishika nafasi ya tano nyuma ya Simba SC, Yanga, Azam na Mtibwa zenye pointi 16.
Kipigo hicho kinahatarisha uhai wa Ruvu Shooting kwenye ligi hiyo hasa kutokana na nafasi yao, kwa sasa kikosi hicho kinashikilia mkia baada ya jana Kagera Sugar iliyokuwa mkiani kwa muda mrefu kushinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC na kupanda hadi nafasi ya 13