CRISTIANO RONALDO AWA MWANASOKA WA DUNIA

CRISTIANO Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani, FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu 2017 ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.

Mchezaji huyo kutoka Ureno amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki kwa mwaka kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La liga, na Ligi ya Klabu bingwa barani Ulaya.

Ronaldo alipokea tuzo yake mjini London  na aliwashukuru mashabiki wake na wa Real Madrid, wachezaji wenzake na rais wake.

Tuzo kwa mchezaji bora mwanamke ilinyakuliwa na mchezaji wa Uholanzi Lieke Martiens, anayeichezea Barcelona, Martiens aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017

Cristiano Ronaldo mshindi wa Ballon D' Or

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA