Yanga na Stand ni kufa au kupona, Ajibu kuongoza safu ya ushambuliaji
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Leo ndio leo katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wenyeji Stand United wakiikaribisha Yanga SC mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Yanga leo itamtegemea zaidi mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu (Aliyeshikilia jezi namba 10) hasa baada ya kuwaacha Dar es Salaam mastaa wake watatu, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko.
Msimu uliopita katika uwanja huo huo wa Kambarage timu hizo zilipokutana Stand ilishinda bao 1-0 hivyo leo ni zamu ya Yanga kushinda ama laah.
Yanga iliwasili Shinyanga juzi ikitokea Tabora ambako ilicheza mechi ya kirafiki na Rhino Rangers na kulazimishwa sare tasa ya 0-0 lakini ilichezesha kikosi cha pili