Stand United kwachafuka, kocha mkuu asimamishwa
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Baada ya kupokea vichapo mfululizo, Stand United imeamua kumsimamisha kocha wake mkuu, Athuman Bilal maarufu Bilo kwa utovu wa nidhamu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Stand United imesema kuwa wamemsimamisha kocha wao kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
Hali si shwari kwa timu hiyo yenye maskani yake mjini Shinyanga kwani hadi sasa inakamata nafasi ya 15 ikiwa ya pili kutoka mkiani, Stand United ilipokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya mabingwa watetezi Yanga wiki iliyopita na hadi sasa nidhamu kwa wachezaji imeshuka mpaka kumsimamisha kocha huyo.
Katibu mkuu wa timu hiyo Kennedy Mwangi amedai Bilo amesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja na tayari wamemwandikia barua ili aweze kujibu tuhuma zake kabla hawajatoa maamuzi mengine, kwa udadisi wa Mambo Uwanjani imegundua matokeo mabaya ndio chanzo cha kumsimamisha na huenda akafutwa kazi