Kagera Sugar yanusurika kichapo kwa Mwadui
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Timu ya Kagera Sugar inayonolewa na kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita wa 2016/17, Mecky Mexime jioni ya leo imenusurika kipigo toka kwa wenyeji wao Mwadui FC ya bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Mwadui walitangulia kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Poul Nonga aliyeunganisha krosi ya Malika Ndeule na kumpita kirahisi kipa mkongwe Juma Kaseja.
Vijana wa Kagera Sugar walionyesha hasira ya kutaka kusawazisha goli hilo lakini iliwachukua hadi kipindi cha pili dakika ya 87 iliposawazisha bao kupitia kwa Jaffari Salum Kibaya ambaye alitumia vema makosa ya beki wa Mwadui, David Luhende.
Kwa matokeo hayo sasa Kagera wanafikisha pointi tatu bado wanaendelea kubaki mkiani huku hatma ya kocha wao Mecky Mexime iko shakani na inawezekana naye akaondoshwa mapema