YANGA KUUTUMIA UWANJA WAKE WA KAUNDA MSIMU UJAO
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Yanga SC imepanga kuutumia uwanja wake wa Kaunda ifikapo msimu ujao kwa mechi mbalimbali za kirafiki na mashindano.
Pia imebainika kwamba mjumbe mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe bayana kwakuwa si msemaji wa klabu, ameiambia Mambo Uwanjani kuwa maendeleo makubwa ya uwekezaji yanayofanyika sasa, yanaupa hadhi uwanja huo wa Kaunda.
Na msimu ujao Yanga itautumia uwanja huo kwa mazoezi na mechi za kirafiki, lakini pia timu za madaraja mengine kama Daraja la kwanza, daraja la pili na daraja la tatu zitaumia kwa mashindano.