Jeshi la Simba kamili gado kuiangamiza Njombe Mji kesho
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC kesho wanashuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuumana na Njombe Mji FC ya mkoani Njombe mchezo unaotazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kesho jeshi la Simba litaendeleza mauaji yake kama kawaida na wala hakutakuwa na sare ama kupoteza mchezo.
Manara amedai ujio wa Mrundi, Masudi Juma ambaye amekuja kuchukua mikoba ya Jackson Mayanja aliyejiuzuru juzi, inaipa jeuri Simba kushinda mchezo huo wa kesho, Simba ikimaliza mchezo huo itaelekea Zanzibar ambapo inaenda kuweka kambi kujiandaa na mpambano wa watani dhidi ya Yanga SC