Baada ya kupata ushindi wake wa kwanza Ligi Kuu, Mexime aanza kuchonga
Na Mwandishi Wetu. Bukoba
Baada ya kikosi chake cha Kagera Sugar kujikongoja na kupata ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime ameanza kuchonga.
Kocha huyo bora wa VPL msimu uliopita ameanza kutamba akisema kikosi chake kimeanza ligi na Jumamosi ijayo kitaendeleza mauaji kwa maafande wa Tanzania Prisons katika uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kagera Sugar itawakaribisha maafande wa Prisons ambao jana Jumatatu wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani, lakini Mexime amedai ushindi ni lazima na ameahidi kikosi chake kitasogea hadi nafasi za juu kuwania ubingwa