YANGA NA SIMBA NI MECHI YA KUCHANA MIKEKA LEO
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Leo ndio leo ambapo Jamhuri ya muungano wa Tanzania itasimama kwa muda kupisha mpambano wa watani wa jadi Yanga na Simba utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Mechi hiyo ya raundi ya nane Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatajwa itakuwa ya kuchana mikeka kwani kuna watu wamebeti matokeo lakini huenda isiwe hivyo walivyobeti wao kwani matokeo yataamuliwa na dakika tisini.
Katika mchezo huo Yanga huenda ikawategemea zaidi wachezaji wake ambao ni kipa Youthe Rostand, walinzi Juma Abdul na Gardiel Michael, lakini pia itamtumainia kiungo wake Papy Tshishimbi na washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu.
Wakati Simba nao itawategemea zaidi Aishi Manula, Erasto Nyoni, James Kotei, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya, yote kwa yote tusubiri muda ufike kwani mshindi wa leo atakaa kileleni.
Simba wao waliingia Dar es Salaam jana asubuhi wakitokea visiwani Zanzibar kwa ndege ambapo walikaa wiki moja kujiandaa na mchezo huo, Yanga nao wametokea Morogoro ambako nao walikaa siku nne, hivyo mpambano wa leo utakuwa wa kusisimua