Kocha mpya Simba apata kibali cha kazi
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Hatimaye kocha mpya msaidizi wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Masoud Djuma raia wa Burundi amepata kibali cha kufanya kazi nchini ambacho kimetolewa na idara ya uhamiaji.
Djuma aliyejiunga na kikosi hicho Alhamisi iliyopita akichukua mikoba ya Jackson Mayanja aliyejiuzuru kwa matatizo ya kifamilia, alishindwa kukaa benchi na kuishia jukwaani Jumamosi iliyopita Simba ilipocheza na Njombe Mji FC uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Kocha huyo aliyewahi pia kucheza soka kama mshambuliaji akiwa na vilabu vya Rayon Sports na APR zote za Rwanda kabla hajavifundisha vyote viwili, sasa ataanza kazi rasmi Jumamosi ijayo wakati Simba ikicheza na hasimu wake Yanga uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam