Kichuya adhihirisha Yanga hawana mabeki wa kumzuia asifunge

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Ukuta wa Yanga bado unaendelea kudhalilishwa na Shiza Ramadhan Kichuya ambaye jana ameweza kufunga bao lake la tatu dhidi ya Yanga, na yote amefunga katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Shiza Ramadhan Kichuya ambaye ni mtoto wa shabiki wa Yanga anayeishi mkoani Morogoro, amethibitisha kuwa Yanga hawana beki wa kuweza kumzuia kwani amefunga katika mechi tatu na kuifikia rekodi ya Amissi Tambwe ambaye naye ameitungua Simba mara tatu mfululizo.

Kichuya alifunga goli msimu uliopita Oktoba 1 mwaka jana wakati miamba hiyo ilipotoka sare ya 1-1, goli lake lilikuwa la kusawazisha alifunga kwa mpira wa kona, pia akafunga goli la kusawazisha, Simba ikiifunga Yanga 2-1 Aprili mwaka huu na tena amefanya hivyo jana

Shiza Kichuya (Kushoto akimtoka beki wa Yanga, Andrew Vicent "Dante"

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA