MILAMBO YAKIONA CHA MOTO KWA WANAJESHI WA MSANGE
Na Emil Kasapa. Tabora
Timu ya soka ya Msange JKT ya TABORA imewatandika ndugu zao MILAMBO FC ya TABORA katika mchezo wa ligi daraja la pili TANZANIA BARA mchezo ukipigwa katika dimba la Mwinyi mjini hapa.
Goli pekee la dakika ya 46 likifungwa na Hamad Yahaya lilitosha kuwapa ushindi wageni hao wa soka wanaochipukia mkoani hapa na kufuta matumaini ya Milambo ya kushinda mchezo huo
Mchezo huo ni wapili mfululizo kwa MILAMBO kupoteza baada ya kufungwa bao moja kwa bila na MASHUJAA ya Kigoma wiki iliyopita wakati MSANGE JKT wao waishinda bao tano kwa mbili dhidi ya NYANZA ya Manyara.
Baada ya Mchezo huo mwalimu wa Msange JKT,Gift Emmanuel amesema timu yake haikuanza vizuri mwanzoni mwa ligi kwa hakuwepo na kwa sasa mambo yataendelea kuwa mazuri na kuwasihi wanatabora kuhamishia mapenzi kwa timu hiyo.
Kwa upande wake mwalimu Andrew Zoma wa Milambo amesema ni moja ya matokeo ya mpira na anajipanga kwa mzunguko wa pili.
Kwa matokeo hayo MSANGE JKT wamefikisha alama nane na kuwapumulia WANAZUKE MSELEBENDE-MILAMBO FC waliopo nafasi ya pili na alama zao tisa katika kundi D.