Yanga yaijibu Simba, nayo yaigonga Stand United 4-0
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga SC jioni ya leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, ushindi huo ni majibu kwa mahasimu wao Simba ambao jana waliichapa Njombe Mji FC magoli 4-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba na Yanga zitaumana Jumamosi ijayo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara hivyo kila timu imejaribu kushinda kwa kumtumia salamu mwenzie.
Ibrahim Ajibu Migomba alikuwa mwiba kwa vijana wa Stand United akifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuifanya Yanga iende mapumziko ikiwa vinara, kipindi cha pili Yanga waliongeza mabao mengine mawili, Pius Buswita akifunga la tatu na Mzambia Obrey Chirwa akiongeza la nne.
Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha pointi 15 sawa na Simba lakini inaangukia nafasi ya pili na kuishusha Mtibwa Sugar, Yanga sasa inakamata nafasi hiyo kwa wingi wa mabao dhidi ya Mtibwa ambayo ilikuwa inashikilia nafasi hiyo