MRITHI WA MAYANJA AWASILI MSIMBAZI

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Hatimaye mrithi wa Jackson Mayanja ambaye alikuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba amewasili nchini tayari kabisa kujiunga na machampion hao wa kombe la FA na Ngao ya Jamii, Simba SC.

Masudi Juma mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Burundi na kocha mkuu wa Rayon Sports ametua na ameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba na muda wowote kuanzia sasa anamwaga wino kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo akisaidiana na Mcameroon, Joseph Omog.

Kocha huyo amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere mapema leo na amefurahi kuja kufanya kazi katika klabu hiyo akisema Simba ni klabu kubwa barani Afrika hivyo anajiona ni mtu muhimu sana.

Aidha kocha huyo amedai amekuja kuipa mataji Simba ambayo mpaka sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 12 ikicheza mechi sita

Masudi Juma kocha msaidizi mpya wa Simba
Masudi Juma akitua Mwl Nyerere International leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA