Mayanja ataja kikosi cha Stars kitakachoivaa Benin, Novemba 11
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga ametangaza kikosi kamili cha timu ya taifa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.
Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda nchini Benin kucheza na wenyeji Novemba 11 mwaka huu.
Na leo kocha Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.
Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa, Aishi Manula, (Simba SC), Peter Manyika, (Singida United) na Ramadhan Kabwili (Yanga SC), Mabeki ni Boniface Maganga, (Mbao FC), Abdi Banda, (Baroka FC, Afrika Kusini), Gardiel Michael (Yanga SC), Kevin Yondan, (Yanga SC), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni, (Simba SC) na Dickson Job, (Mtibwa Sugar).
Viungo: Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar, Kenya), Mzamiru Yassin, (Simba SC), Raphael Daudi, (Yanga SC), Simon Msuva, (Difaa El Jadida, Morocco).
Wengine ni Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Ajibu (Yanga SC) Mohamed Issa, (Mtibwa Sugar), Farid Musa (Tenerife, Hispania) na Abdul Mohamed, (Tusker, Kenya), washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuf, (Azam FC), Elius Maguri, (Huru) na Yohana Nkomola (Huru)