Sare dhidi ya Yanga, Simba wambebesha lawama mwamuzi

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Baada ya kushindwa kulinda goli lao na hatimaye Yanga kusawazisha na matokeo kuwa 1-1 , vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC wamemtulia lawama mwamuzi aliyechezesha mechi ya watani Simba na Yanga, Jumamosi iliyopita uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Heri Sasii kwa kushindwa kuwazawadia penalti mbili wakati wachezaji wawili wa Yanga waliunawa mpira kwenye maeneo hatari.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara 'Computer' amesema mwamuzi Heri Sasii aliwabeba Yanga waziwazi kwa kushindwa kuwapa penalti, anasema beki wa Yanga, Kevin Yondan na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi walinawa mpira kwa nyakati tofauti na video imeonyesha matukio.

Manara analalamikia kitendo cha mwamuzi huyo kuwanyima waziwazi Simba penalti akidai imekuwa kawaida Yanga kupendelewa na waamuzi, hata hivyo Yanga ilisawazisha goli katika dakika ya 60 likifungwa na Obrey Chirwa baada ya Simba kutangulia kufunga.

Simba ilijipatia bao lake ya kuongoza dakika ya 57 lililofungwa na Shiza Kichuya, kipa wa Simba Aishi Manula alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya wachezaji wa Yanga iliyokuwa inaenda wavuni moja kwa moja

Haji Manara 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA