LIGI KUU KUENDELEA TENA KESHO, MWADUI NA KAGERA KAZI IPO
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Kesho Ijumaa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena kwa mchezo mmoja tu utakaozikutanisha Mwadui FC na Kagera Sugar katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi ambapo Mbao FC vs Azam FC, CCM Kirumba Mwanza, Lipuli vs Majimaji Songea, Samora Stadium, Iringa, ilihali Ruvu Shooting vs Mbeya City, Sokoine, Mbeya na Simba vs Njombe Mji uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ndanda FC vs Singida United, Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons, Manungu Complex Morogoro.
Wakati Jumapili Stand United vs Yanga SC, CCM Kambarage mjini Shinyanga, Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 12 wakifuatiwa na Mtibwa Sugar, Yanga na Azam zote hizo zina pointi 12