Chirwa ainusuru Yanga kulala kwa Simba
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Goli la kusawazisha lililofungwa kunako dakika ya 60 jioni ya leo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, limetosha kabisa kuipa sare ya bao 1-1 na mahasimu wao Simba SC.
Hadi mapumziko timu hizo zimeenda vyumbani zikiwa hazijafungana hata bao, kwa hakika leo mpira umepigwa mwingi karibu timu zote mbili lakini Papy Kabamba Tshishimbi ameendelea kuwa nyota wa mchezo kwa mara ya pili.
Yanga watajilaumu sana kwa kushindwa kuchomoza na ushindi kufuatia mashambulizi yao ya kushutukiza, Shiza Kichuya aliifungia Simba bao la uongozi dakika ya 58, timu hizo sasa zote zikifikisha pointi 16.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho ambapo viwanja sita vitawaka moto lakini mchezo utakaozikutanisha Mtibwa Sugar na Singida United utakaofanyika uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro unatajwa kuwa mkali na wa kusisimua