Bocco kuikosa Njombe Mji
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC leo wataendelea kumkosa straika wake hatari John Bocco 'Adebayor' ambaye ana maumivu na atakaa nje kwa wiki moja, taarifa iliyotolewa na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara hivi karibuni imesema straika huyo atakaa nje.
Simba inakutana na Njombe Mji jioni ya leo ya leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kukosekana kwa straika huyo kunafifisha ndoto za vinara hao kuendelea kukaa kileleni kwani kama itateleza kwa kutoka sare tena ama kufungwa basi itaondolewa kileleni.
Katika siku za hivi karibuni Simba imekuwa ikipata ushindi mwembamba kutokana na washambuliaji kushindwa kuzitumia vema nafasi