Azam FC yaishusha Simba kileleni usiku huu

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku huu wamefanikiwa kukamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, baada ya kuilaza Mbeya City ya mkoani Mbeya bao 1-0 uwanja wa Azam Complex usiku huu.

Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana hata bao, kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini Azam FC wakafanikiwa kujipatia goli la ushindi.

Goli hilo lililofungwa kunako dakika ya 59 na mshambuliaji wake Mbaraka Yusuf aliyeitendea haki pasi nzuri ya Mghana, Enock Atta Agyei, kwa ushindi huo Azam sasa inakuwa kileleni kwa kuishusha Simba iliyokuwa inaongoza ligi, Azam wamefikisha pointi 16 lakini wamecheza mechi nane.

Hata hivyo Azam FC itakaa kileleni kwa masaa tu kwani kesho inaweza kuondolewa kileleni na Simba, Yanga au Mtibwa ambazo zitashuka dimbani

Azam FC wamekaa kileleni usiku huu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA