Yanga nao watua Dar na kuelekea hotelini tayari kuua mnyama kesho

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC wamewasili mchana wa leo wakitokea mkoani Morogoro ambapo waliingia kambini tangu Jumanne iliyopita wakitokea Shinyanga ambako waliishinda Stand United mabao 4-0 Jumapili iliyopita mchezo wa Ligi Kuu bara.

Machampioni hao wa kandanda wametua mchana ea leo kwa basi na moja kwa moja wameelekea hotelini ambapo watakaa hadi kesho na saa wataelekea uwanja wa Uhuru jijini kwa ajili ya kuua mnyama, Yanga inakutana na hasimu wake Simba na kikubwa kwao ni kulipiza kisasi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti Agosti 23 mwaka huu mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii.

Hata hivyo msemaji wa Yanga Dissmas Ten,hakuweka wazi hoteli gani waliyofikia akidai wanahofia hujuma kutoka kwa watu wasiowatakia mema, katika mchezo wa kesho Yanga inaweza kuwakosa nyota wake watatu Wazimbabwe  Thabani Kamusoko na Donald Ngoma lakini pia itamkosa na Mrundi Amissi Tambwe

Wachezaji wa Yanga wakirejea mchana wa leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA