Yanga yazaliwa upya, Manji awatisha Simba
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi ijayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Yanga SC wanaingia katika mchezo huo wakiwa na ari na kasi mpya hasa baada ya aliyekuwa mwenyekiti wao na mfadhili mkuu, bilionea Yusuf Manji kuungana na wachezaji wa kikosi hicho na akiwaahidi neema endapo watashinda mechi zao zote za mzunguko wa kwanza ukiwemo dhidi ya Simba.
Manji amewaambia wachezaji hao kuwa yeye ni Mwanayanga na anahitaji furaha hivyo wapambane walete ushindi Jumamosi ijayo watakapoumana.
Kibopa huyo aliyefutiwa kesi zake zote mbili, kwa sasa yuko huru na amejitolea kuwalipa mishahara wachezaji wote na wale wanaoidai klabu hiyo huku akisema bado yupo Yanga, hayo ni maneno ya kuudhi kwa wapenzi wa Simba.