SIMBA YAITUMIA SALAMU YANGA, YAIGONGA NJOMBE 4-0
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Simba SC jioni ya leo imewatumia salamu mahasimu wao wakuu Yanga SC, baada ya kuilaza Njombe Mji FC mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo mkubwa unazidi kuisogeza zaidi kileleni kwa kufikisha pointi 15 na mabao ya kufunga 17 huku mshambuliaji wake Emmanuel Okwi ambaye leo ametupia goli moja na kuseti mawili akizidi kuongoza kwa kufunga mabao manane.
Simba leo ilicheza vizuri kwa maelewano makubwa na kufanikiwa kupata bao moja hadi filimbi ya kuelekea mapumziko ilipopulizwa, kipindi cha Simba ilirejea na makali zaidi ikifanikiwa kufunga magoli matatu na kuondoka na pointi tatu muhimu.
Magoli mengine ya Wekundu hao wa Msimbazi, yalifungwa na Muzamir Yassin (mawili) na Laudit Mavugo aliyemalizia goli la nne, kikosi hicho cha Simba kesho kitaelekea Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mpambano wa watani dhidi ya Yanga, Jumamosi ijayo