Buffon aula kikosi cha FIFA

SHIRIKISHO la soka duniani, FIFA limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka jana 2016.

Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpo World xi, Mlinda mlango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan ya Italia, Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya mkongwe wa Barcelona, Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi.

Mshambuliaji mpya wa PSG, Neymar Jr raia wa Brazil, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa hapa duniani naye ameingia kuchukua nafasi ya Luis Suarez katika safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi hicho bora cha ulimwengu.

Hakuna hata mchezaji mmoja wa ligi ya premia (EPL) aliyefanikiwa kujumuhishwa katika kikosi hicho.

KOCHA BORA DUNIANI

Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea, Antonio Conte baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda La liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili mfululizo.

Conte alishinda ligi ya premia msimu uliopita, naye Massimiliano Allegri wa Juventus ambaye aliiongoza klabu yake kushinda Serie A na Coppa Italia msimu uliopita alikuwa wa tatu katika kinyang' anyiro hicho.

Katika kura zilizopigwa ambazo zilimpa ushindi Zidane nyota wa zamani wa Barcelona na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa zilikuwa kama ifuatavyo: Zinedine Zidane 46.22% Antonio Conte 11.62% na Massimiliano Allegri 8.78%

Gianluigi Buffon amemshinda Manuel Neuer katika kikosi cha Fifa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA