Saa za Omog zinahesabika Simba, apewa mechi mbili
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa Simba SC, Mcameroon, Joseph Marius Omog yuko shakani kusalia kikosini na muda wowote anarejea nyumbani huku Mrundi Masoud Djuma akichukua nafasi yake.
Omog amepewa mechi mbili tu na ikitokea bahati mbaya Simba ikapoteza mechi moja kati ya hizo ama kutoka sare basi kibarua chake kitafutwa rasmi, Simba ililazimishwa sare ya 1-1 na mtani wake Yanga lakini ilielemewa na kuomba mpira uishe.
Vigogo wa Simba hawakufurahishwa na matokeo hayo isitoshe Simba msimu huu imefanya usajili mkubwa kuliko timu zote, mashabiki wa Simba pia hawamtaki kocha huyo wakidai ameshusha kiwango cha Simba.
Simba iko kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga huku timu nne Simba, Yanga, Mtibwa na Azam zote zina pointi sawa 16 kila moja na mechi 8, Omog sasa amepewa mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Prisons zote itacheza ugenini jijini Mbeya