SIMBA WATUA KIBABE DAR, WAENDA KUJIFICHA SERENA, KESHO KUIFYEKAFYEKA YANGA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC wamewasili asubuhi ya leo katika uwanja wa kimataifa wa ndege (JNIA) wakitokea Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki moja tayari kabisa kumkabili mtani wake wa jadi Yanga SC mchezo wa Ligi Kuu bara utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utapigwa kesho utaanza saa 10:00 jioni na mwamuzi wa kati atakuwa kijana Heri Sasii ambaye ana beji ya Fifa, wachezaji wa Simba walipotua moja kwa moja wakaingia kwenye basi lao na kuelekea katikati ya jiji ambapo watakaa katika hoteli ya kifahari ya Serena na kesho wataenda kuifyekafyeka Yanga.
Wachezaji wa Simba wametua kwa shauku kubwa uwanjani hapo leo na kila mchezaji ameonekana katika hali ya kujiamini, Simba inakwenda kuendeleza ubabe kwani ikumbukwe tangia Februali 20 mwaka 2016 hawajafungwa tena Yanga na wameweza kushinda mechi tatu mfululizo na zote za mashindano