Tutaisimamisha Simba kesho, asema kocha wa Njombe Mji
Na Ikram Khamees. Mlandizi
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Njombe Mji, Mrage Kabange amesema vijana wake wataingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kesho kwa kazi moja tu ya kuisimamisha Simba katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Njombe Mji tangu ilipomtimua kocha wake mkuu Hassan Banyai, haijapoteza mchezo wowote na kesho imepania kuondoka na pointi, Kabange amesema anaijua vizuri Simba hivyo kazi yake itakuwa moja tu, kuizuia.
Njombe Mji wameweka kambi yao Mlandizi mkoani Pwani, lakini kesho watachuana na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC mchezo ambao utatoa mwelekeo wa vilabu vyote viwili.
Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja alibwaga manyanga juzi Jumatano na nafasi yake ilichukuliwa na Mrundi, Masudi Juma ambaye zamani alikuwa akiinoa Rayon Sports ya Rwanda, kwa maana hiyo mechi hiyo itakuwa na rekodi za kipekee kwa timu zotembili