BOCCO, MO FITI KUIVAA YANGA, JUMAMOSI
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar
Washambuliaji John Raphael Bocco "Adebayor" na Mohamed Ibrahim "Mo" sasa wako fiti na Jumamosi ijayo wataiongoza timu yao ya Simba katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga, uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba kwa sasa wapo Zanzibar wameweka kambi kujiandaa na mchezo huo na wachezaji hao ambao walikuwa majeruhi wamepona na walianza mazoezi tangu jana na kuendelea leo na kwa mujibu wa daktari wa timu Yassin Gembe amesema wako fiti.
Gembe amesema Simba itaendelea kuwakosa Shomary Kapombe, Said Mohamed Nduda na Salim Mbonde ambao ni majeruhi wa muda mrefu, kupona kwa Bocco na Mo kunaweza kukaipa ahueni kubwa Simba ambayo itajivunia uwepo wa nyota hao