BAADA YA GEORGE WEAH KUSHINDA URAIS LIBERIA, ATHUMAN CHINA NAYE KUWANIA URAIS TANZANIA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mwanasoka wa zamani nchini, Athuman China ambaye aliwahi kuzichezea Yanga na Simba pamoja na Taifa Stars anayeishi nchini Uingereza ametangaza azma yake ya kugombea urais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa nyakati zijazo.
China anafuata nyayo za mkongwe Leodegar Tenga ambaye amewahi kuliongoza shirikisho hilo, Tenga naye aliwahi kuzichezea kwa nyakati tofauti, Yanga, Pan Africans na timu ya taifa.
Akizungumza kutoka Uingereza, China amesema nia yake kuja kuukomboa mpira wa Tanzania ambao unazidi kudidimia, kiungo huyo wa zamani aliyetamba vilivyo amesema watu wa mpira kama yeye ndio watakaoweza kuuokoa