Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2017

AJIBU AWASHANGAA SINGIDA UNITED

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajibu Migomba anawashangaa Singida United kwa kitendo cha kumtangaza kwamba wanataka kumsajili wakati hawajawahi kumwita mezani. Ajibu anashindwa kuwaelewa viongozi wa Singida United timu iliyopanda Ligi Kuu mwaka huu, Akizungumza Mambo Uwanjani, Ajibu amesema mkataba wake na Simba unamalizika mwezi ujao hivyo yuko tayari kusaini kokote. Amedai Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm imeweka wazi mipango yake ya kumsajili Ajibu lakini bado haijafanya mazungumzo naye hivyo nyota huyo anaweza kuota mbawa

Hivi ndivyo beki wa zamani wa Simba alivyoagana na ukapela

Picha
Beki wa zamani wa Simba SC, Salum Mpakala "Distance" hivi karibuni alifunga ndoa na kuachana na ukapela, Mpakala aliwahi kuichezea Simba miaka ya 2003 hadi 2004 wakati Simba ikitikisa. Baada ya kuachana na Simba, nafasi yake akasajiliwa Salum Kanoni, Mpakala alisajiliwa na Simba akitokea Vijana ya Ilala sambamba na kipa Haji Macharazi. Baada ya kuachana na Simba nyota huyo alienda Namibia sambamba na Madata Lubigisa kucheza soka la kulipwa kisha akatimkia Sweden ambako alikaa mpaka mwaka jana aliporejea Dar es Salaam na kuendelea na maisha mengine nje ya soka

Mecky Mexime akubali kutua Yanga

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mecky Mexime wa Kagera Sugar amekubali kibarua cha kumsaidia kocha mkuu wa Ysnga Mzambia George Lwandamina. Hivi karibuni kulikuwepo na taarifa kwamba Klabu ya Yanga inataka kumnasa Mexime ambaye aliiongoza vema timu ya Kagera Sugar na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya msimu huu uliomalizika. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa kocha mkuu wa Yanga Mzambia George Lwandamina anamuhitaji Mexime ili awe msaidizi wake badala ya Juma Mwambusi. Baada ya kuzisikia taarifa hizo, kocha Mecky Mexime amekubali kuwa kocha msaidizi wa Yanga akiamini ni timu kubwa na hapo ni sehemu sahihi kwake kujiendeleza kitaaluma, amewaomba Yanga wamfuate na kuingia naye kandarasi kwani hiyo ni kazi yake

Shose wa Simba kuagwa Alhamisi

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Yule shabiki wa Klabu ya Simba Shose Fideris aliyefariki katika ajali ya gari iliyotokea Dumila mkoani Morogoro ambapo ndani yake alikuwemo nahodha wa Simba Jonas Mkude ataagwa Alhamisi ijayo. Shabiki huyo ataagwa Alhamisi kuanzia saa 5:00,asubuhi katika hospitali ya Mwananyamala kisha saa 7:00 mchana katika kanisa katoliki Magomeni, na atasafirishwa mkoani Kilimanjaro na kuzikwa Ijumaa, marehemu Shose alifariki wakati gari alilopanda akitokea Dodoma kutazama mchezo wa fainali kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC. Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-1 na kutwaa kombe la FA, Wakiwa njiani kurejea Dar es Salaam wakisafiri na gari aina ya Range Cluiser V8 iliyokuwa ikiendeshwa na Ahmed Kassim "Rais wa Kibamba" ambaye ndiye mmiliki, lilipasuka tairi la mbele kuingia porini Kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani Publishers inatoa salamu za pole kwa familia ya Shose na wapenzi na mashabiki wa Simba SC

Atupele Green rasmi Singida United

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kagera Sugar na JKT Ruvu, Atupele Green Jackson amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Singida United iliyopanda Ligi Kuu. Atupele ambaye timu yake ya JKT Ruvu imeshuka daraja, ameamua kujiunga na Singida iliyokuwa ikimuhitaji, Singida United imekuwa ikijiimarisha kwenye usajili na tayari imeshawanasa wachezaji sita mpaka sasa wenye uzoefu. Kutua kwa mshambuliaji huyo ambaye mwaka jana aliibuka mfungaji bora kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA, ila mwaka huu tuzo hiyo amenyang' anywa na Mzambia Obrey Chirwa wa Yanga ambaye ndiye mfungaji bora. Wakati huo huo beki wa Mbao Fc ya Mwanza, Asante Kwasi ameigomea ofa ya Singida United na kuweka wazi mipango yake ya kutaka kujiunga na Azam FC, Asante Kwasi kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake kwenye timu hiyo ya Mbao

Masikini Mkude! Atemwa Stars

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Nahodha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jonas Gerald Mkude ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakachoondoka kesho kuelekea Cairo Misri kwa ziara ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Lesotho Juni 10. Akizungumza leo, Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Alfred Lucas amesema Mkude ameenguliwa kwenye kikosi hicho kutokana na ushauri wa madaktari hasa baada ya kupata ajali. Mkude alipata ajali jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kupinduka maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi wanne akiwemo yeye huku mwenzao mmoja, Shose Fideris kuaga dunia. Mkude aliiongoza Simba kutwaa ubingwa wa kombe la FA baada ya kuilaza Mbao FC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma juzi, na wakiwa njiani na gari lao aina ya Range Cluiser V8 lilipasuka tairi na kuhama njia

Aishi Manula kukaribia kutua Singida United

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Singida United imeweka wazi mpango wake wa kumnasa Tanzania One, Aishi Manula ambaye mkataba wake na Azam FC unaelekea ukingoni. Mmiliki wa Singida United, Yusuph Mwandeni ameiambia Mambo Uwanjani kuwa timu yake inajidhatiti kwenye suala la usajili na sasa kiu yao ni kuona kipa huyo mahiri wa Taifa Stars anatua kwao msimu ujao. Singida United mpaka sasa imeshasajili wachezaji watano wa kimataifa, na majuzi imemsajili kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally, Singida United ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi Kuu Bara, nyingine zilizopanda ni Njombe Mji na Lipuli ya Iringa

Malinzi amlilia Shose wa Simba

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Klabu ya Simba kufuatia msiba wa mpenzi na shabiki wake Shose Fideris. Shose alifariki dunia jana katika ajali ya gari iliyotokea Dumila mkoani Morogoro, gari aina ya Range Cluiser iliyokuwa ikiendeshwa na Ahmed Kassim au Rais wa Kibamba kama anavyofahamika kupasuka tairi na kutokomea porini. Ndani ya gari hilo pia alikuwemo nahodha wa Simba Jonas Mkude ambaye aliumia sambamba na dereva na watu wengine wawili, Mkude na wenzake walitokea Dodoma ambako juzi Simba ilicheza fainali na Mbao Fc na kushinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa FA Cup kwenye uwanja wa Jamhuri. Wakiwa njiani ndipo ajali hiyo ilipotokea na kusababisha kifo cha shabiki huyo kindakindaki wa Simba, Malinzi amewapa majeruhi wa ajali hiyo na akisikitishwa na kifo cha shabiki huyo

BANDA ANAKWENDA AFRIKA KUSINI, AKIDUNDA KUSAINI YANGA

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Kiungo wa Simba anayemudu kucheza pia beki ya pembeni, Abdi Hassan Banda Jr, jana aliwaaga wapenzi na mashabiki wa Simba kwamba anaondoka zake katika timu hiyo kwenda kujaribu changamoto nyingine kwingineko. Imefahamika kwamba kiungo huyo aliyewahi pia kuzichezea African Sports na Coastal Union zote za Tanga, anataka kwenda kujaribu bahati yake nchini Afrika Kusini lakini dili ikibuma anasaini Yanga miaka miwili. Rafiki wa mchezaji huyo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake amedai Banda anaenda Afrika Kusini ambapo alitakiwa na klabu moja ya huko lakini ishu hiyo ikibuma anasaini Yanga. Banda aliwaaga mashabiki wa Simba jana kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Mbao FC ambapo Simba ilishinda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa, mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Shabiki kindakindaki wa Simba aliyefariki ajalini Dumila

Picha
Na Mwandishi Wetu. Morogoro Jumapili ya Mei 28 imetokea ajali mbaya ya gari maeneo ya Dumila mkoani Morogoro ambapo gari aina ya Range Cluiser V8 inayomilikiwa na shabiki mwingine wa Simba Ahmed Kassim "Rais wa Kibamba" kupata ajali mbaya na kusababisha kifo cha mwanadada Shose Fideris. Kwa mujibu wa mashabiki wa Simba waliojitokeza kusaidia kuokoa majeruhi akiwemo nahodha na kiungo wa Simba, Jonas Gerald Mkude na mmiliki wa gari na abiria wengine, Shose alifariki papo hapo, ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo kupasuka tairi la mbele na kuingia porini. Mipango ya kuuleta mwili wa shabiki huyo kindakindaki wa Simba ambayo jana ilitwaa ubingwa wa kombe la FA kwa kuilaza Mbao FC katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Simba ilishinda mabao 2-1 Shose Fideris enzi za uhai wake Nahodha wa Simba Jonas Mkude akiwa na madaktari mara alipofikishwa hospitalini Gari walilopatia ajali akina Mkude na marehemu Shose

JONAS MKUDE ANUSURIKA KIFO DUMILA

Picha
Na Ikram Khamees. Morogoro Nahodha wa Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC, Jonas Gerald Mkude amenusurika kifo katika ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo ya Dumila mkoani Morogoro. Mkude na wenzake watano akiwemo mwanachama maarufu wa Klabu hiyo ambaye ndiye mmiliki wa gari hilo Ahmed Kassim kwa jina maarufu Rais wa Kibamba waliumia vibaya baada ya gari lao Range Cluiser V8 kuhama njia na kutokomea porini baada ya tairi la mbele kupasuka. Mashabiki wa Simba waliokuwa wakitokea mkoani Dodoma kuangalia fainali ya kombe la FA ambapo ilichezwa jana na timu ya Simba kutwaa ubingwa baada ya kuilaza Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 2-1 walijitokeza kuwasaidia majeruhi wa ajali hiyo akiwemo Mkude. Hata hivyo hali ya afya ya Mkude inaimarika na wala hajaumia sana anaendelea vizuri huku inadaiwa katika ajali hiyo kulikuwemo na abiria mmoja wa kike aliyefahamika kwa jina la Shose mkazi wa Dar es Salaam amefariki dunia kwenye ajali hiyo na mwili wake umehifadhiwa hospitalini na utasafirishwa Dar es...

Everton kutua Dar es Salaam Juni

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya Everton ya Uingereza itawasili jijini Dar es Salaam mwezi ujao na itacheza mechi yake ya kirafiki katika Uwanja wa Taifa, vigogo hao wa Uingereza wataletwa nchini na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa. Kwa mujibu wa tovuti ya Everton imesema kwamba, timu hiyo itatua Dar es Salaam kwa mwaliko wa Sportpesa na watacheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu itakayochukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 5 mwaka huu. Bingwa wa michuano hiyo mbali na kujinyakulia kikombe na shilingi Milioni 60, pia atapata fursa ya kucheza na Everton moja kati ya timu zinazosumbua Uingereza

Sanchez, Ramsey waing' arisha Arsenal England

Picha
Magoli mawili yaliyofungwa na Alexis Sanchez na Aoron Ramsey yalitosha kabisa kuipa ushindi Arsenal wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa fainali ya kombe la FA Uwanja wa Wembley London. Sanchez alitangulia kufunga bao la kwanza kabla ya Diego Costa kuisawazishia Arsenal kwa bao maridadi lililotokana na juhudi zake binafsi, Lakini Aoron Ramsey alikatisha matumaini ya Chelsea kutaka kuongeza kikombe cha pili msimu huu baada ya kufunga bao la ushindi. Bao hilo lilifungwa dakika ya 79 na liliwapa ubingwa Arsenal ambao msimu huu wamemaliza katika nafasi ya tano EPL, Mkufunzi wa Arsenal, Arsenel Wenger alifurahia ubingwa huo wa FA na kusema msimu huu alikutana na changamoto nyingi na anashukuru vijana wake hawakumwangusha

SIMBA MABINGWA WAPYA FA CUP 2016/17 WAIDUWAZA MBAO 2-1

Picha
Na Ikram Khamees. Dodoma Mabao mawili yaliyofungwa na Muivory Coast, Fredrick Blagnon na Shiza Ramadhan Kichuya (Penalti) yametosha kabisa kuipa Simba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Mchezo huo ulimalizika ndani ya dakika 120 baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo timu hizo zikiwa 0-0, lakini katika dakika za nyongeza ikashuhudiwa magoli yote yakipatikana, Blagnon alikuwa wa kwanza kuifungia Simba bao la kuongoza kabla ya Mbao FC kusawazisha. Shiza Kichuya zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kumalizika akaipatia Simba bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penalti uliotokana na mchezaji wa Mbao kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, kwa matokeo hayo Simba wanakuwa mabingwa wapya na watashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika mwakani. Pia Simba itaambulia shilingi Milioni 50 ambazo bingwa hujinyakulia, Hata hivyo wachezaji wa Mbao FC walimshutumu mwamuzi wa mchezo ...

Mlemavu wa mapenzi ya Viso iko hewani

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Msanii chipukizi wa miondoko ya Bongofleva, Vincent Patrick "Viso' ameitambulisha nyimbo yake mpya inayofahamika kwa jina la Mlemavu wa Mapenzi aliyoirekodi katika studio za Jini Sounds zilizopo Tabata Shule jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Mambo Uwanjani leo, Viso amesema wimbo huo una mahadhi ya bongofleva na anaamini utafanya vizuri kwenye vituo vya redio, msanii huyo amemsifu prodyuza wake Nalo ambapo amemsifu kwa kudai ameutendea haki wimbo huo. Mbali na kuachia wimbo huo redioni, Viso anajipanga kuachia wimbo mwingine ambapo amesema nao ni wimbo mkali, "Wimbo huu niko katika mikakati ya kuutengenezea video, mashabiki wangu wakae mkao wa kula, Viso nakuja kivingine", alisema huku akitabasamu

"RASTA" KAMUSOKO AITWA TIMU YA TAIFA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kiungo wa kimataifa wa Yanga SC, Thabani Scara Kamusoko "Rasta" ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe kinachojiandaa na mchezo wa mataifa Afrika dhidi ya Liberia mwezi ujao. Kocha mkuu wa Zimbabwe, Norman Mapeza amemjumuhisha kiungo huyo fundi wa Yanga SC mabingwa wa Tanzania Bara kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa, Kamusoko anakuwa Mzimbabwe wa kwanza kwa wanaocheza Ligi Kuu ya Bara kuitwa timu ya taifa. Akimzungumzia Kamusoko, Mapeza amesema ameamua kumuita kwenye kikosi chake baada ya kuridhishwa na kiwango chake akiwa na Yanga SC hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho. "Kamusoko ni mmoja kati ya viungo bora ambao wanafaa kuitumikia Zimbabwe", alisema Mapeza ambaye anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Liberia

Rufaa ya Simba FIFA utata mtupu

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Imeelezwa kuwa Klabu ya Simba imeshindwa kuwasilisha rufaa yake ikitaka ipewe ushindi wa mezani wa pointi tatu kutoka kwa Kagera Sugar, Simba ilifungwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Inadaiwa Kagera Sugar ilimchezesha Mohamed Faki ambaye alikuwa na kadi tatu za manjano kwa maana hiyo Simba walistahili kupewa pointi tatu na mabao mawili licha ya kipigo hicho, awali Simba ilipeleka malalamiko yake Bodi ya Ligi na ikapewa pointi tatu na mabao mawili. Baadaye Kagera Sugar nao walikata rufaa TFF kupitia kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ambapo ikaamua kuwarudishia pointi tatu zao na mabao mawili kwa moja, pointi hizo kama Simba ingebaki nazo sasa hivi ndo wangekuwa mabingwa wa Tanzania Bara kwakuwa wangekuwa na pointi 71. Baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika viongozi wa Simba wakatuma Fax yao FIFA wakitaka shauri lao lisomwe upya na wao wapewe pointi tatu, lakini kwa mujibu wa FIFA, haiwezekani timu kupewa ubingwa wa mezan...

Ni fainali ya maajabu Simba na Mbao FC

Picha
Na Ikram Khamees. Dodoma Uwanja wa Jamhuri Stadium mjini Dodoma ambako ni makao makuu ya serikali itapigwa fainali ya aina yake Jumamosi ya Mei 28 kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Mbao FC vijana wanaocheza kandanda la hali ya juu wanaotokea jijini Mwanza. Maajabu ya fainali hiyo ni kwamba endapo Mbao FC itashinda mchezo huo basi itakuwa timu ya kwanza kutoka mikoani kuwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa mwakani, Mbao itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Mchezo huo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFA) maarufu kombe la FA utakuwa na maajabu mengi ikiwemo Simba kupata tiketi ya kuwakilisha taifa kwa mara ya kwanza baada ya kukosa kwa miaka minne mfululizo. Timu zote mbili zina vikosi imara na yeyote anaweza kuchomoza na ushindi, Mbao FC mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoka kuitoa nishai Yanga baada ya kuilaza bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, pia utakuwa ni mchezo wa kisasi kwani Mba...

Yanga watua kwa Gardiel Michael wa Azam

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, sasa vilabu kadhaa vimeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao, Klabu bingwa ya soka nchini Yanga SC imeanza kubisha hodi kwa Azam FC na kutaka kumng' oa mlinzi wake wa pembeni Gadiel Michael. Habari ambazo mtandao huu umezipata zinasema kuwa Yanga imeridhishwa na kiwango cha mlinzi huyo ambaye ameonyesha kiwango kikubwa msimu uliomalizika wa 2016/17 ingawa timu yake ya Azam kukamata nafasi ya nne. Yanga wanataka kumchukua mlinzi huyo aliyemaliza mkataba na klabu hiyo na uhakika wa kutua Yanga unaonekana ni mkubwa, Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwamdamina anataka kumtumia zaidi Gadiel kwani hakuridhishwa na Mwinyi Hajji ambaye amekuwa akipoozesha mashambulizi

BOCCO AMWAGA WINO MSIMBAZI

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mshambuliaji hatari wa Klabu Bingwa Afrika mashariki na kati pamoja na kombe la Mapinduzi, Azam FC, John Raphael Bocco "Adebayor" amesaini mkataba wa miaka miwili katika timu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi. Bocco amemwaga wino huo tayari kabisa kuitumikia Simba msimu ujao, nyota huyo akisifika mno akiwa katika kikosi cha Azam hasa kwa kuzitungua klabu kubwa na kongwe za Simba na Yanga. Awali Yanga ilivumishwa kutaka kumsajili lakini baadaye dili la kujiunga nao likaishia njiani na Simba wakamalizana naye jana, Uongozi wa Azam FC haujawa tayari kuelezea kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Bocco alizaliwa mwaka 1989 jijini Dar es Salaam na amekuwa mmoja kati ya washambuliaji bora katika miaka ya hivi karibuni

Infatinho alipoikatia umeme Simba SC

Picha
Jana kulizuka taarifa mitandaoni kwamba Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani ameitumia salamu za pongezi Klabu Bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC kupitia kwa Rais wa Shirikisho la kandanda Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi. Taarifa hizo zilionekana kupuuzwa na mahasimu wa Yanga, Simba SC ambao walisikika wakisema kwamba zimetengenezwa na watu wa Yanga, wanadai FIFA  haiwezi kuwatumia salamu Yanga kwakuwa Simba imekata rufaa ikitaka ipewe pointi za chee dhidi ya Kagera Sugar. Lakini kwa mujibu wa TFF taarifa hizo za salamu za Rais wa FIFA, Gian Infantinho ni kweli ameitumia salamu TFF kwa kukamilisha vema Ligi Kuu ya soka ya Tanzania na kumpata bingwa mpya ambaye ni Yanga SC

Haruna Niyonzima alivyowabwaga wageni wenzake

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima (Pichani) raia wa Rwanda, jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17. Niyonzima alishinda tuzo hiyo kwa wachezaji wa kigeni ambapo ameweza kuwaangusha nyota wenzake wanaotoka nje, Niyonzima alidhihirisha hilo pale alipojitokeza kuisaidia Klabu yake kutwaa ubingwa wa Bara kwa msimu huu. Mchango wake ulikuwa ukionekana uwanjani ambapo anapokosekana pengo lake lilijionyesha dhahili na pale anapoingia makali yake huonekana, Niyonzima ni nahodha msaidizi wa Yanga pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi Stars

Simba SC ilivyopokelewa Dodoma Leo

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dodoma Klabu ya soka ya Simba leo iliwasili mjini Dodoma na kupata mapokezi makubwa kama unavyoona pichani, Simba imewasili Dodoma ikiwa tayari kwa mchezo wa fainali dhidi ya Mbao FC Jumamosi ijayo katika uwanja wa Jamhuri Stadium. Mchezo huo wa kuwania ubingwa wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la TFF, Gumzo ni mchezo huo kwani bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Simba iliingia fainali baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Azam FC kwa bao 1-0 wakati Mbao FC iliifunga Yanga SC bao 1-0, je ni nani atakayeibuka na ushindi katika mchezo huo?

Yanga ilivyozoa mamilioni ya ubingwa VPL

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Klabu bingwa Tanzania Bara, Yanga SC jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City walitunukiwa tuzo yao ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17. Yanga walipewa kitita chao cha shilingi Milioni 84 wakiwa kama mabingwa wa msimu huu, huo ni ubingwa wake wa 27 na wa tatu mfululizo kwao

Mourinho aibebesha taji la Ulaya Man United

Picha
Tangu alipoondoka Mscotland Alex Ferguson katika kikosi cha Manchester United ya Uingereza, mambo yalikuwa hovyo kabisa alipotua Mscotland mwenzake David Moyes ambapo timu hiyo ilipoteza heshima yake. Wengi walidhani ujio wa Luis Van Gaal raia wa Uholanzi mambo yangekuwa safi kwakuwa kocha huyo aliiongoza vema timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia michuano iliyofanyika nchini Brazil. Ujio wa Mreno Jose Mourinho katika kikosi cha Manchester United pia wengi hawakutarajia maajabu ingawa kocha huyo amekuwa na maajabu mengi, tayari kocha huyo ameipa mataji matatu timu hiyo ila taji kubwa kabisa ni la Ulaya. Jana usiku Man United imetwaa ubingwa wa kombe la Ueropa League baada ya kuilaza Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa mabao 2-0, hayo ni mafanikio makubwa kwa kocha huyo aliyewahi pia kuziongoza, Inter Milan, Chelsea na Real Madrid

Pale Mexime alipowaduwaza makocha wa kigeni na kutwaa tuzo

Picha
Na Saida Salum. Mlimani City Kocha Mecky Mexime wa Kagera Sugar jana usiku alitwaa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17. Mexime ameiongoza Kagera Sugar na kufanikiwa kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya miamba Yanga SC waliotwaa ubingwa na Simba SC waliokamata nafasi ya pili. Kutwaa kwa tuzo hiyo kwa mzalendo huyo, kumewafanya makocha wa kigeni wa timu za Simba na Yanga kushindwa kuambulia tuzo yoyote mbele yake, shukrani kwake Mecky Mexime ambaye aliwahi pia kuinoa Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro

Mbaraka Yusuf Abeid mchezaji bora chipukizi VPL

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mshambuliaji chipukizi wa Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera, Mbaraka Yusuf Abeid usiku wa jana katika ukumbi wa Mlimani City Hall jijini Dar es Salaam alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa msimu uliomalizika wa 2016/17 ambapo timu yake imemaliza katika nafasi ya tatu. Mbaraka alikuwa mmoja kati ya washambuliaji chipukizi waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo kiasi kwamba aliweza kuzichachafya Simba na Yanga, Mbaraka alifunga kwenye mechi zote mbili alizokutana na Simba pamoja na Yanga. Pia chipukizi huyo aliitwa timu ya taifa, Taifa Stars na aliweza kufunga bao muhimu ambalo liliipa ushindi Stars wa mabao 2-1 dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Singida United yaibomoa Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya Singida United ya mkoani Singida imeendelea kuimarisha kikosi chake hasa baada ya kubisha hodi kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na kumnasa kipa wake Ally Mustapha "Barthez". Taarifa zenye uhakika ambazo Mambo Uwanjani haizitilii shaka zinasema kuwa Singida Unied iko mbioni kumpa mkataba wa miaka miwili kipa huyo ambaye amekuwa na bahati mbaya katika kikosi cha Yanga kwani hakutumika karibu msimu mzima. Tayari Singida United imeshamnasa kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, timu hiyo inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm na msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza

Tshabalala awa mchezaji bora wa VPL

Picha
Na Saida Salum. Mlimani City Tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilinyakuliwa na mlinzi wa pembeni wa Simba SC Mohamed Hussein "Tshabalala" au Zimbwe Jr kama mwenyewe anavyojiita. Tuzo hiyo ilitolewa usiku wa leo ambao pia ulihusisha tuzo kwa wachezaji wengine na vilabu, Yanga SC wenyewe waliondoka na tuzo tatu ikiwemo yao ya kutwaa ubingwa wa Bara na kuambulia kitita cha shilingi Mil 84. Simon Msuva na Haruna Niyonzima waliing' arisha Yanga kwa kujizolea tuzo, Msuva alichukua tuzo ya ufungaji bora sambamba na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting wakati Haruna Niyonzima yeye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kigeni. Wengine waliobeba tuzo ni Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wakati Mecky Mexime alishinda tuzo ya kocha bora

Sportpesa yazigonganisha Simba na Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa imetangaza kuanzisha michuano yake ya soka kwa ukanda huu wa Afrika mashariki itakayoshirikisha timu kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kenya. Michuano hiyo itafahamika kwa jina la Sportpesa Super Cup na itaanza Juni 5 mwaka huu, timu zote zinazodhaminiwa na kampuni hiyo ndizo zitakazoshiriki ambazo ni Yanga, Simba na Singida United kwa upande wa Bara. Nyingine ni Nakuru All Star, Gor Mahia, Tusker FC na AFC Leopards zote za Kenya wakati Jang' ombe Boys ya Zanzibar nayo itashiriki michuano hiyo ambayo itafanyikia jijini Dar es Salaam, lengo na madhumuni ya kampuni hiyo ni kuendeleza soka la Afrika mashariki

Jk amfuata Samata Ubelgiji

Picha
Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samata anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji. Kikwete yupo Ubelgiji kuhushuria mkutano wa kimataifa kuhusu Libya na ikumbukwe yeye ndiye msuluhishi wa mgogoro wa nchi hiyo iliyopo Afrika ya Kaskazini, (Pichani JK akiteta na Samata)

Sportpesa yamwondoa Manji Jangwani

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kitendo cha Klabu Bingwa Tanzania Bara, Yanga SC kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa kimepelekea mwenyekiti wake Yusuf Mehbood Manji kujiuzuru wadhifa wake huo. Manji ameandika barua ya kujizuru jana Mei 22 na amesema anawashukuru Wanayanga kwa mshikamano wao tangu alipoingia kwenye klabu hiyo miaka 16 iliyopita, Manji tangu alipochaguliwa kuiongoza klabu hiyo imetwaa ubingwa wa Bara misimu yote na kutengeneza kikosi bora ambacho kiliwahi kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho. Inasemekana kiongozi huyo ameamua kujiuzuru kwa sababu ya mkataba wa Sportpesa ambao utazifanya jezi za Yanga kuitangaza kampuni hiyo badala ya Quality Group, uamuzi huo wa Yanga kuingia mkataba na kampuni hiyo halikuwa pendekezo lake isipokuwa ni wazo la watu wachache ambao walitaka kuingia ndani ya Yanga hasa baada ya yeye kuyumba alipokuwa na matatizo na serikali

Msuva na Mussa kulamba zawadi ya mfungaji bora VPL

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Jamal Emili Malinzi amesema tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara maarufu VPL itakwenda kwa Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting. Wachezaji hao wote wawili wamefunga mabao 14 kila mmoja na kuwafanya wagawane zawadi ya mfungaji bora inayotolewa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya simu Vodacom. Tuzo zinatarajiwa kutolewa Mei 24 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,

Yanga bingwa 2016/17

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Yanga SC ya Dar es Salaam leo imefanikiwa kuweka rekodi ya miaka kadhaa baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara licha ya kufungwa bao 1-0 na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Yanga imetwaa ubingwa huo baada ya kushuka uwanjani mara 30 ikifikisha pointi 62 ambazo zimefikiwa na mahasimu wao Simba SC waliopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Baadhi ya matokeo ya mechi nyingine ni Kagera Sugar 1 Azam Fc 0, Mtibwa Sugar 3 Toto Africans 1, matokeo mengine tutaendelea kuwajuza lakini Toto Africans, African Lyon na JKT Ruvu zimeshuka daraja

Kakolanya aitwa Stars, Dida atemwa

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amemjumuhisha kipa wa Yanga, Benno Kakolanya katika kikosi chake chenye wachezaji 23 ambacho kitaingia kambini kabla ya kuelekea Misri ambako itaenda kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Lesotho Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mayanga amemwita Kakolanya ambaye amecheza vizuri katika kikosi cha Yanga hivi karibuni na kuamua kumtema kipa mzoefu Deogratus Munishi "Dida" pia wa Yanga. Katika orodha ya kikosi hicho cha Stars kitakachoshiriki michuano ya kombe la Cosafa itakayofanyika mwezi ujao nchini Afrika Kusini kimejumuhisha makipa wanne Aishi Manula (Azam FC) na Said Mohamed wa Mtibwa Sugar. Nyota wengine waliojumuhishwa ni Hassan Kessy, Mwinyi Haji Mngwali (Yanga), Mohamed Hussein "Tshabalala", Abdi Banda (Simba), Salim Abdallah, Agrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni (Azam FC). Wengine ni Himid Mao, Salum Abubakar "Sure Boy (...

Serengeti wanusa kombe la Dunia

Picha
Na Mwandishi Wetu. Libreville Tanzania imepiga hodi Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 Oktoba mwaka huu India baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola jioni ya leo katika mchezo wa Kundi B fainali za U-17 Afrika Uwanja wa L' Amitie mjini Libreville, Gabon. Ushindi huo unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi 4 na kukaa kileleni mwa kundi B, baada ya kucheza mechi mbili ya kwanza ikitoa suluhu 0-0 na Mali Jumatatu ya wiki hii. Katika mchezo huo uliochezeshwa na Abou Coulibaly kutoka Ivory Coast aliyesaidiwa na Mamady Tere wa Guinnea na Attla Amsaad wa Libya hadi mapumziko kila timu ilikuwa na bao moja. Tanzania walitangulia kea bao la mshambuliaji tegemeo Yohana Mkomola dakika ya tano baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi, Francisco Chilumba aliisawazishia Angola. Kipindi cha pili Serengeti waliongeza bidii na kufanikiwa kuongeza bao la pili na la ushindi lililofungwa na Abdul Seleman na kuifanya Tanzania inuse fainali za kombe la Dunia zitakazofan...

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL hawa hapa

Picha
Wachezaji watano wameteuliwa (nominees) kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017. Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga). Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini. Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu. Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Dogo Mfaume afariki dunia

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Habari mbaya kwa mashabiki wa muziki wa miondoko ya Mchiriku hasa kufuatia kifo cha staa aliyetamba na wimbo matata "Kazi yangu ya dukani", Dogo Mfaume. Taarifa za kuenea kwa kifo chake zilienea mapema leo ila Mambo Uwanjani haijapata undani zaidi na itaendelea kuwajuza mara tu itakapopata habari kamili. Mungu amlaze mahara pema peponi, Amina

Stars yaangukia mikononi mwa Angola, Cosafa Cup

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa kundi A katika michuano ya mataifa ya Afrika yaliyo ukanda wa kusini maarufu Cosafa Cup ambayo yanatarajia kuanza mwezi ujao. Kwa mujibu wa waandaaji wa michuano hiyo, Cosafa inaonyesha Stars imeangukia kundi A litakalokuwa na timu nne wakati kundi B nalo lina timu nne, hii ni mara ya pili kwa Stars kushiriki michuano hiyo yenye msisimko mkubwa tofauti na michuano ya Chalenji inayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika mashariki. Katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Afrika Kusini, Stars imepangwa na Angola, Malawi na Mauritius mataifa mengine manne yatakayokuwa kundi B ni Msumbiji, Zimbabwe na Shelisheli

Yanga nao waingia mkataba na Sportpesa miaka mitano

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini Yanga SC wameingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya bahati nasibu ya Sportpesa wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.173 za Kitanzania. Mkataba huo kati ya Yanga na Sportpesa utaifanya Yanga ichukue shilingi Milioni 950 kwa mwaka, hii itawafanya wawalipe mishahara wachezaji wake bila matatizo yoyote. Ujio wa Sportpesa umeleta faraja kwa vilabu vya Simba na Yanga ambavyo sasa vitaanza kujiendesha vyenyewe kuliko hapo nyuma ambapo viliendesha kwa fedha za watu

Toto wamebana wameachia, Tambwe awapa ndoo ya tatu Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Bao lililofungwa kunako dakika ya 81 na mshambuliaji Amissi Tambwe raia wa Burundi, jioni ya leo limetosha kabisa kuwapa ubingwa wa tatu mfululizo Yanga SC dhidi ya watoto wao Toto Africans. Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ushindi wake wa 1-0 umeifanya Yanga ifikishe pointi 68 na michezo 29 sawa na vilabu vyotw vinavyoshiriki ligi hiyo. Haikuwa kazi rahisi kwa Yanga kujipatia bao la ushindi kwani vijana wa Toto Africans "Wana Kishamapanda" leo walistahili pongezi kwa kuwabana vilivyo baba zao Yanga SC na kuwalazimisha suluhu ya 0-0 hadi mapumziko. Kipindi cha pili pia kilikuwa kigumu kwa Yanga kwani mabeki wa Toto walifanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Obrey Chirwa wasifanye madhara langoni mwao, Kipa wa Toto David Kisu leo alikuwa kikwazo kwa Yanga kwa kuokoa magoli kadhaa. Mabadiliko yaliyofanywa na Yanga ya kumtoa Geofrey Mwashiuya na kumwingiza Emmanuel Martin viliisaidi...

Msuva kuikosa Toto leo

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Winga wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Simon Msuva atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Toto Africans Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Msuva anaukosa mchezo huo muhimu ambao unaweza kumpa ama kumnyima tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Msuva anaongoza kwa mabao akiwa amefunga mabao 14 akifuatiwa na Abdulrahaman Mussa. Msuva aliumia eneo la usoni wakati akifunga bao wakati Yanga ikiilaza Mbeya City mabao 2-1, Msuva alifunga bao kwa jitihada zake binafsi na kwa bahati mbaya aliumizwa katika harakati za kufunga. Endapo Yanga itashinda katika mchezo wa leo itakuwa imefikisha pointi 68 na itakuwa tayari imeshajihakikishia ubingwa wa Bara

Serengeti Boys waanza kwa sare Gabon

Picha
Na Ikram Khamees. Libreville Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya  Tanzania maarufu Serengeti Boys jioni ya leo imewalazimisha sare ya 0-0 mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali katika mchezo wa kwanza kundi B Uwanja wa I' Amitie Sino jijini Libreville. Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja na Mali walionekana kuutawala muda wote lakini shukrani pekee ziwaendee mabeki wa Serengeti Boys ambao walifanya kazi ya ziada na kulinda muda wote. Wachezaji wa Mali ambao wana uzoefu mkubwa na michuano hiyo walishindwa kuupita ukuta wa Serengeti na kumaliza mchezo kwa sare na wakiambulia pointi moja