"RASTA" KAMUSOKO AITWA TIMU YA TAIFA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kiungo wa kimataifa wa Yanga SC, Thabani Scara Kamusoko "Rasta" ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe kinachojiandaa na mchezo wa mataifa Afrika dhidi ya Liberia mwezi ujao.
Kocha mkuu wa Zimbabwe, Norman Mapeza amemjumuhisha kiungo huyo fundi wa Yanga SC mabingwa wa Tanzania Bara kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa, Kamusoko anakuwa Mzimbabwe wa kwanza kwa wanaocheza Ligi Kuu ya Bara kuitwa timu ya taifa.
Akimzungumzia Kamusoko, Mapeza amesema ameamua kumuita kwenye kikosi chake baada ya kuridhishwa na kiwango chake akiwa na Yanga SC hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho.
"Kamusoko ni mmoja kati ya viungo bora ambao wanafaa kuitumikia Zimbabwe", alisema Mapeza ambaye anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Liberia