Aishi Manula kukaribia kutua Singida United
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam
Singida United imeweka wazi mpango wake wa kumnasa Tanzania One, Aishi Manula ambaye mkataba wake na Azam FC unaelekea ukingoni.
Mmiliki wa Singida United, Yusuph Mwandeni ameiambia Mambo Uwanjani kuwa timu yake inajidhatiti kwenye suala la usajili na sasa kiu yao ni kuona kipa huyo mahiri wa Taifa Stars anatua kwao msimu ujao.
Singida United mpaka sasa imeshasajili wachezaji watano wa kimataifa, na majuzi imemsajili kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally, Singida United ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi Kuu Bara, nyingine zilizopanda ni Njombe Mji na Lipuli ya Iringa