Mlemavu wa mapenzi ya Viso iko hewani
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Msanii chipukizi wa miondoko ya Bongofleva, Vincent Patrick "Viso' ameitambulisha nyimbo yake mpya inayofahamika kwa jina la Mlemavu wa Mapenzi aliyoirekodi katika studio za Jini Sounds zilizopo Tabata Shule jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mambo Uwanjani leo, Viso amesema wimbo huo una mahadhi ya bongofleva na anaamini utafanya vizuri kwenye vituo vya redio, msanii huyo amemsifu prodyuza wake Nalo ambapo amemsifu kwa kudai ameutendea haki wimbo huo.
Mbali na kuachia wimbo huo redioni, Viso anajipanga kuachia wimbo mwingine ambapo amesema nao ni wimbo mkali, "Wimbo huu niko katika mikakati ya kuutengenezea video, mashabiki wangu wakae mkao wa kula, Viso nakuja kivingine", alisema huku akitabasamu