Simba SC ilivyopokelewa Dodoma Leo
Na Mwandishi Wetu. Dodoma
Klabu ya soka ya Simba leo iliwasili mjini Dodoma na kupata mapokezi makubwa kama unavyoona pichani, Simba imewasili Dodoma ikiwa tayari kwa mchezo wa fainali dhidi ya Mbao FC Jumamosi ijayo katika uwanja wa Jamhuri Stadium.
Mchezo huo wa kuwania ubingwa wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la TFF, Gumzo ni mchezo huo kwani bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Simba iliingia fainali baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Azam FC kwa bao 1-0 wakati Mbao FC iliifunga Yanga SC bao 1-0, je ni nani atakayeibuka na ushindi katika mchezo huo?