Serengeti wanusa kombe la Dunia
Na Mwandishi Wetu. Libreville
Tanzania imepiga hodi Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 Oktoba mwaka huu India baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Angola jioni ya leo katika mchezo wa Kundi B fainali za U-17 Afrika Uwanja wa L' Amitie mjini Libreville, Gabon.
Ushindi huo unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi 4 na kukaa kileleni mwa kundi B, baada ya kucheza mechi mbili ya kwanza ikitoa suluhu 0-0 na Mali Jumatatu ya wiki hii.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Abou Coulibaly kutoka Ivory Coast aliyesaidiwa na Mamady Tere wa Guinnea na Attla Amsaad wa Libya hadi mapumziko kila timu ilikuwa na bao moja.
Tanzania walitangulia kea bao la mshambuliaji tegemeo Yohana Mkomola dakika ya tano baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi, Francisco Chilumba aliisawazishia Angola.
Kipindi cha pili Serengeti waliongeza bidii na kufanikiwa kuongeza bao la pili na la ushindi lililofungwa na Abdul Seleman na kuifanya Tanzania inuse fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika Oktoba mwaka huu nchini India, mchezo mwingine kwenye kundi B ni kati ya Niger na Mali